Singida Town Center Church (STCC) ni kanisa la
Pentekoste Singida, ni mama wa makanisa yote ya FPCT mkoa wa Singida, na ndilo
kanisa la kwanza la kipentekoste katika mji wa Singida. Jengo hili
ambamo leo tunafanyia ibada lilikuwa ni
kanisa la Kitlutheri, na hili ndilo kanisa la kwanza katika mji wa Singida.
Jengo hili lilijengwa mwaka 1936.
Kanisa hili Lilianzia
katika katika kijiji cha Unyanga, kitongoji cha Isingo mwaka 1963 mwezi juni.
Baadae kanisa lilihamia mjini Singida katika eneo la mitunduruni ambako nyumba
moja ilinunuliwa, Mchungaji alikaa hapo na ibada zikafanyikia hapo (kwa bahati
mbaya nyumba hii iliuzwa mwaka 1995 kwa ajili ya ujenzi wa kanisa la Kibaoni).
Mwaka 1970 kanisa
lilihama kutoka Mitunduruni na kuhamia katika eneo la Ipembe- katikati ya mji
wa Singida (yaani hapa tulipo). Jengo hili, awali lilikuwa kanisa la kilutheri,
jengo hili lilinunuliwa kutoka kwa Walutheri kwa thamani ya Shilingi 23,700/-
na fedha hizo za kununulia jengo hili
zilitolewa na mtumishi wa Mungu kutoka Denmak anayeitwa Paul Paulsen (sasa
hayupo duniani tena).
Kuanzia hapo kanisa
lilipanuka na kusambaa katika mkoa mzima wa Singida na kufanya leo takribani
kila kijiji kuwa na kanisa la Pentekoste. kutoka katika kanisa hili, kuna
watumishi wengi waliosambaa nchi nzima,wakifungua kazi mpya. Na wengine
wanafanya kazi ya utume nje ya Tanzania.
Kanisa lilianzishwa na Wamissionari kutoka katika kanisa la
Herning-Denmark naye ni missionari
Alfred Jensen na Mke wake Ulla, mwaka 1962 alipokuwa Sanjaranda Alfred aliota
ndoto ya kuanzisha kazi mpya katika mji wa Singida, ndipo mwezi juni 1963
alifika Singida na kuanzisha kanisa hili.
Wamisionari wengine waliofanyakazi hapa Singida
kutoka Denmark ni pamoja na Peter Madsen na mke wake Anne Lise (Baba yake
Torben Madsen), Egon Falk na mke wake Hanner, Over Petersen na mke wake Dorrit,
Eve Boeson, kutoka Norway
ni Gudbrad Sanvord na mke wake Inger, na kutoka Uingereza ni Nigel
Double na mke wake Barbara na Anthony
Williams na mke wake Elizabeth.
Mchungaji wa kwanza mzalendo ni Mchungaji Zephania Mtinangi (marehemu),
akifuatiwa na Andrea Duma (marehemu), akifuatiwa na wengine wengi, hatimaye mchungaji Mathayo
Timo makhata mwaka 1986 hadi 1992 na sasa
Dr.Paul Samweli mwaka1992 hadi leo.
Kanisa hili tangia kuanzishwa kwake mwaka 1963
liliungana na makanisa mengine ya pentekoste katika Tanzania yaliyokuwa
yakifanya kazi chini ya Muungano uliokuwa ukijulikana kama Umoja wa makanisa ya
pentekoste Tanzania (UMPT), (Chini ya UMPT kila kanisa la mahali lilikuwa na
usajiliwa wake) Lakini mwaka 2000 makanisa yalikubaliana kutengeneza katiba
moja na kuwa na kanisa moja lenye usajili moja ambalo sasa linalojulikana kama ‘’The Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT)’’ lililosajiliwa mwaka
2000 kwa Namba SO 6640 na Wizara ya Mambo ya Ndani Ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania. Kwa maana hiyo sasa kanisa la
Pentecoste Singida (STCC) linafanya kazi chini ya kanisa la mahali la
Singida la The Free Pentecostal Church
of Tanzania (FPCT).
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
1 comments:
MUNGU WETU WA MBINGUNI AWABARIKI KWA MAONO YA KUITUNZA HISTORIA YA KANISA LETU KTK BLOG.
ReplyPost a Comment